Mtumaini Bwana sikuzote, Maana Bwana Yehova ni mwamba wa milele.@Isaya 26:4
picha
Augustus M. Toplady (1740-1778)

Augustus M. Toplady, 1776 (Rock of Ages); . Hatujui kama ni kweli, lakini vile tumeambiwa bwana Toplady aliandika maneno haya kama alijificha kutoka upepo kali na mwua, chini ya mwamba, karibu na Cheddar Gorge kwa Ulaya; Wanasema aliandika maneno haya kwa karatasi kidogo, yaani karata.

Thomas Hastings, 1830 (🔊 pdf nwc).

Mwamba wenye imara,
Kwako nitajificha.
Maji na damu yako,
Toka mbavuni mwako,
Iwe dawa ya kosa,
Kutakasa mioyo.

Si kazi za mikono,
Ziletazo wokovu.
Nikitoa machozi,
Nikifanya kwa bidii,
Siwezi kujiosha,
Unioshe wewe tu.

Sina la mikononi,
Naja msalabani.
Ni uchi, nipe nguo,
Dhaifu, nipe nguvu,
Niondolee taka,
Nitakase sijafa.

Nikaapo dunia,
Nifikapo kifoni.
Nitakapofufuka,
Nitakapokuona,
Mwamba wangu wa kale,
Kwako nitajificha.