Hakuna mtu mwenye upendo unaozidi ule wa mtu anayejitoa afe kwa ajili ya rafiki zake.@Yohana 15:13

Joseph M. Scriven, 1855 (What a Friend We Have in Jesus); .

Charles C. Converse, 1868 (🔊 pdf nwc).

Yesu kwetu ni Rafiki,
Hwambiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye
Maombi asikia;
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya;
Kwamba tulimwomba Mungu
Dua angesikia.

Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia.
Hakuna mwingine mwema
Wakutuhurumia;
Atujua tu dhaifu;
Maombi asikia.

Je, hunayo hata nguvu,
Huwezi kwendelea,
Ujapodharauliwa
Ujaporushwa pia.
Watu wangekudharau
Wapendao dunia,
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia.